Je nisome kozi Gani ????
** Uchambuzi wa kina kuhusu utofauti wa IT, Computer science, Computer Engineering, Software engineering na Cyber security.** Post hii nimewandalia hususan wanafunzi waliomaliza sekondari wakitarajia kwenda vyuoni kusomea kozi za computer ila kwa sababu ya ugeni wa elimu ya chuoni pamoja na muda mfupi wa kufanya maamuzi, wanapata wakati mgumu wa kujua ni kozi ipi ya kuchagua itayowafaa. Kukosea kuchagua kozi sahihi ni ajali kama ajali zingine … kukosea kuchagua kozi unaweza kukutana na vitu ndivyo sivyo ulivyodhania, kozi ukikosea kuichagua unaweza kumaliza chuo na hakuna ajira zake hapa bongo, kozi ukikosea kuchagua unaweza ukawa umeparamia vitu ambavyo vimekuzidi uwezo na kupelekea usome kwa kutumia nguvu kubwa sana hata kwenye vitu ambavyo ni basic, hii itafanya elimu yako chuoni iwe ya mateso makali kupelekea uwe unafanya mitihani ya marudio (ku supp) na endapo ukishindwa mitihani hii unajiongezea mzigo wa masomo ya ziada kwa kuanza upya kuyasoma darasa...