SOMA HII IKUSAIDIE
Kama unahisi simu imepotea mahali ulipo ndani ya dakika chache ( chini ya dakika 15 angalau), jaribu hatua za kuipigia, kama imezima jaribu kuingia katika simu au computer ya jirani (nyingine) na ku log in katika account zako ili endapo ikiwashwa na ikawa na internet uweze kuitrack kwa kutumia
Andika Find my device na Google – kama ni Android, au
Find katika iCloud – kama ni iOS
Block line zako za simu, unaweza kufanya hivi kwa kufika katika duka la mtandao wako lililopo karibu yako.
1.Report Polisi.
Na ki ukweli Polisi sio sehemu rahisi sana kupeleka mambo yako haraka kama ambavyo ungependa na zaidi Polisi kuna sheria zake na muda wake lakini hii ndiyo njia pekee ya uhakika ya jinsi ya kupata simu iliyopotea au kuibiwa.
Polisi pekee ndiyo wanaweza kukupa uhakika wa 79% wa kuipata simu yako, hata miezi na miaka baada ya kupotea.
Kwanini Polisi na sio App au watu wengine? ๐ค๐ค๐ค
Mara nyingi wengi waliopotelewa na simu walikuwa hawaja install app zinazoweza kuwasaidia kupata simu zao endapo zitapotea.
App nyingi za kupata simu iliyopotea zinahitaji uwe umeshawahi kuzi install katika kifaa kabla hakijapotea au kama ukiweza kupata access katika kifaa husika.
Unaweza kusoma hii Jinsi ya kulinda simu yako inapopotea, kabla ya kupotea.
Sasa shida ni kwamba watu wengi hawachukui tahadhari, usiwaze kama simu yako imepotea ukifuata taratibu za Polisi bado una uwezo wa kuipata hata baada ya muda na kwa kutumia vitu kama IMEI nk
Oooh yah, IMEI …
Kwa nini IMEI haitoshi wewe kupata simu?
Utakutana na watu wengi wakikwambia kuwa ukiwa na IMEI unapata simu kwa kuitrack online.
Ni kweli kuna uwezekano huo lakini
Sio wa uhakika, mara nyingi inahitaji uwe ulishainstall app.
Ni njama ya matapeli/watu wanaotaka kujipatia pesa kidogo kutokana na shida yako ndo maana watakwambia Just EMEI inayodha.
Apps nyingi zitakupa matangazo tu lakini zinajaribu ku track simu uliyoinstall na sio uliyopoteza bila ku install.
Hata ikiwepo huwa na gharama kubwa.
Najua kama nakuchanganya lkn ndo Ukubwa huo๐๐ soma Makala mpaka mwisho.
Ili tuelewe labda tuangalie IMEI inatumikaje kutambua simu.
IMEI kwa ufupi ni kama namba ya cheti(ID) ya simu.
Kila simu ni lazima iwe nayo na haiwezi kufanana katika simu nyingine.
Unapowasha simu, simu inatafuta mtandao na kuunga katika mtandao wako uliopo karibu zaidi na wewe.
Mtoa huduma wa mtandao mfano Airtel, Vodacom, Tigo anaweza kujua kuwa sehemu fulani kuna mtu fulani ameunga katika mtandao wetu kupitia mnara fulani au fulani kama ni simu isiyo na GPS lakini kama simu ina GPS inaweza kuonesha sehemu sahihi inapopatia mtandao.
Kwa mantiki hii, mtandao wa simu yako mfano Vodacom, Tigo ndio wanaweza zaidi kujua uko wapi, lakini hawawezi kamwe kutoa taarifa hii, otherwise uwe Polisi au uwe na kibali maalumu.
Hii ndio maana Polisi ni sahihi zaidi kukupatia simu.
Changamoto lakini sio hiyo pekee ya kuhitaji Polisi katika hili. Katika namna moja ni lazma huyu mtu atatoa line yako.
Unahitaji Polisi kwa sababu ndio wenye uwezo wa kuomba na kupata taarifa za simu ya IMEI fulani imeonekana wapi na wapi.
Na kama umepoteza simu, relax kwanza usipanick, funga line zako, kisha fuatilia na Polisi, mkiamua wewe na Polisi mtaipata simu.
Na bahati nzuri ukimpata muhusika anatakiwa kukurudishia gharama ulizotumia na zaidi kama ukitaka.
Natuai mpaka hapo Sina la ziada Bye๐๐๐