Je ,????wajua hiiii
IT wengi wa Tanzania wakikosa ajira serikalini kazi ndio imeishia hapo wataenda kujiajiri vitu vingine kabisa, huwa hawawezi kujiajiri kwa ujuzi wa IT sababu hawana skills za IT bali wamekariri vitu vingi kwenye notes pasipo ujuzi, kimbililio pekee kwa IT wengi huwa ni kupata ajira serikalini maana huko vitu vingi ni simple kama kubadili mausi, kubadili keyboard, kupiga window, n.k. mshahara kila mwezi upo. Kwa watu mnasosomea hizi kozi nawajuza tu kwamba ajira za IT serikalini bado ni chache sana hivyo ni heri ujiandae uwe na ujuzi wowte wa IT ili uweze kujiajiri humo humo baada ya kumaliza chuo. Chuoni hata iweje lazima utakuwa na muda wa kupumzika na kufanya mambo yako, huwezi soma masaa yote ambayo hulali labda uwe umechagua kozi ambayo unailazimisha, Hakikisha unajifunza skills zozote iwe ni weekend ama ukipata muda, sehemu nzuri ya kujifunzia ni kwa wale waliojiajiri ambao tayari wanafanya hizi mishe, hakikisha unajenga connections humo ujiunge groups zao, ufahamiane nao na uwe tayari kwenda kufanya kazi nao bure kabisa kwa kujitolea iwe ada yako ya kukusanya maarifa ya ujuzi. Photo studio - ndio fursa basic kabisa ambayo mwana IT, nina marafiki kibao wanaendesha maisha yao kupiga picha, kuzi retouch, n.k. kwa miaka ambayo upo chuoni utengene japo weekend uwe unaenda kwenye studio ujitolee bure kabisa huku wewe unaingiza maarifa, ni rahisi sana kujifunza ukiwa na walipo kwenye kazi. soko kubwa la hizi mambo huwa ni wanawake, wanapenda sana picha hawa dada zetu. Printing and graphics designing - Nina mdogo wangu kamaliza IT hana kazi ila nilimshahuri hizi vitu akiwa chuoni, hakosi laki 1 kila wiki kuandaa kava za wasanii wakitoa ngoma, Hapa uwe na ujuzi wa graphics zaidi, kuna kuandaa mabango, vipeperushi, kadi za mialiko, kava za wasanii, n,k. ukienda kujitolea kufanya kazi kwa wanaodili na haya mambo unapata a to z mambo yanavyokwenda, kama kwenu mpo fresh ukipewa mtaji unanunua printer zako unaanza kazi ukijua kabisa wapi pa kupata wateja, usimamizi, n.k. Kutengeneza laptops - Inawafaa zaidi watu wanaosomea Computer engineering sababu ni kozi ya umeme na hardware za computer, Unaanza taratibu kwa vitu kama kubadili hard disk, kubadili ram, kupukuta na kusafisha laptops, mdogo mdogo utajikuta unaanza kufix shoti kwenye laptops, kubadili button, n.k. Gaming and games - Si biashara ya kuichukulia poa kama wengi wanavyodhani, ni biashara mojawapo inayoweka vijana mjini hii, jifunze kuchipu ps, jifunze kuweka games za pc na ps, n.k. looh !! utapata wateja hawa wapenda games wengi tu, mimi nikiwa chuoni nilikuwa napata wateja kibao wa kuwaingizia games za mpira sema enzi hizo nilikuwa nafanya free, kwa wenye mitaji kuanzia walau milioni 3 hivi wanaweza kufungua vibanda vyao vya kuchezesha games, location nzuri huwa ni karibu na vyuoni, wanachuo wanapenda sana games. Kutengeneza Apps na websites - Fanya kutembelea hubs za haya mambo ili kupata muongozo, ukipata muongozo ni rahisi sana kuliko kuanza kujitaftia mitandaoni sababu mitandaoni utashauriwa kwa mazingira ya ulaya ila hapa ni Tz. n.k